Picha inayodai kuonyesha Emmanuel Nchimbi, Makamu wa Rais wa zamani wa Tanzania, akimfariji Rais Samia Suluhu Hassan katika ikulu kufuatia kifo cha mumewe, imebainika kuwa imehaririwa. PesaCheck ilifanya uchunguzi na kugundua kuwa picha asili inamuonyesha Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akimfariji Rais Samia nyumbani kwake Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 11 Septemba 2026.
Rais Samia alifiwa na mumewe, Hafidh Ameir Hassan, tarehe 7 Septemba 2026. Hassan alifariki akipokea matibabu hospitalini Zanzibar. Viongozi wa ngazi ya juu na watu mashuhuri kutoka Tanzania na nchi zingine za Afrika walimtembelea Rais Samia ili kumfariji kufuatia kifo cha mumewe. Viongozi wengine wa kikanda walitoa jumbe za rambirambi kupitia taarifa zilizoandikwa au matangazo.
Picha ilisambaa mtandaoni mnamo tarehe 23 Septemba 2026, ikidai kumuonyesha Nchimbi akimtembelea Rais Samia ili kumfariji. Hata hivyo, PesaCheck iligundua kuwa picha hiyo imefanyiwa marekebisho. Sheikh Ponda aliondolewa kwenye picha ya awali na nafasi yake kuchukuliwa na Nchimbi. Hakuna taarifa rasmi kuhusu Nchimbi kumtembelea Rais Samia katika ikulu ili kumfariji.
Nchimbi alitangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wa makamu wa rais mnamo tarehe 25 Agosti 2026. Tarehe 26 Agosti 2026, siku moja baada ya kutangaza kujiuzulu kwake, Nchimbi alifukuzwa rasmi kutoka chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Kufuatia kujiuzulu kwake, Nchimbi ametoweka kabisa katika nyanja ya umma.
Bunge la Tanzania tayari limemthibitisha Deogratius Ndejembi kuwa makamu wa rais mpya. PesaCheck imechunguza picha inayodaiwa kumuonyesha Nchimbi akimfariji Rais Samia na kugundua kuwa imehaririwa. Chapisho hili ni miongoni mwa muendelezo wa makala ya kuangalia ukweli ya PesaCheck kwa ajili ya kubaini maudhui yanayoweza kua habari za uongo katika mtandao wa Facebook na mitandao mingine ya kijamii.
PesaCheck ni mradi wa kwanza Afrika mashariki katika maswala ya kuangalia ukweli juu ya pesa za umma. Kwa pamoja ulianzishwa na Catherine Gicheru na Justin Arenstein, mradi upo chini ya Code for Africa shirika kubwa barani linaloongoza katika nyanja ya teknolojia ya urai na uandishi habari wa data. PesaCheck inafanya kazi kusaidia umma kubaini ukweli katika matangazo ya umma yanahusu namba zinazojenga ulimwengu wetu.
Mradi wa PesaCheck unaendelea kusaidia umma kubaini ukweli katika taarifa za umma, hasa katika masuala ya fedha za umma. Kufahamu zaidi kuhusu mradi, tembelea pesacheck.org. PesaCheck ni mradi wa Code for Africa, kupitia mpango wake wa innovateAFRICA fund, kwa msaada kutoka Deutsche Welle Akademie, na ushirikiano na muunganiko wa vyombo vya habari vya ndani vya kiafrika pamoja na mashirika mengine ya kiraia.
Key points
- Picha inayoenezwa mtandaoni ikidai kuonyesha Emmanuel Nchimbi akimfariji Rais Samia imehaririwa.