Mahakama Kuu ya Kenya Jijini Nairobi imetoa uamuzi wa kumfikisha Twaha Mwaipaya, mtanzania aliyekutwa na watu wasiojulikana katika eneo la Kamulu, kaunti ya Machakos, karibu na Jiji la Nairobi, akiwa hai au amekufa. Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Alexander Muteti aliyesikiliza maombi ya dharura yaliyofunguliwa na Taasisi ya Vocal Africa. Mwaipaya anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa katika magari matatu, moja likiwa ni Toyota Landcruicer Hardtop, Jumapili ya Oktoba 25, 2026.

Mwaipaya ambaye ni mwanaharakati na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alikuwa akisafiri na taksi kwenda kusalimia rafiki zake ndipo alizuiwa na watu hao na wakaondoka naye. Tangu kutekwa kwake, jitihada za kumtafuta zimefanyika zikishirikisha Shirika la Amnesty International tawi la Kenya, wanaharakati na Chadema lakini hazijazaa matunda hadi kufikia sasa na hajulikani alipo na katika hali gani.

Hii ndio iliifanya taasisi ya Vocal Africa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kutetea haki za Binadamu nchini Kenya, kufungua maombi hayo Mahakama Kuu kwa hati ya dharura dhidi ya IGP na watu wengine 13. Katika uamuzi wake alioutoa leo Oktoba 30, 2026, Jaji Muteti amesema Maombi yaliyowasilishwa kwa njia ya Chambea (chamber summons), Oktoba 27, 2026, yanathibitishwa hapa kuwa ya dharura.

Jaji Muteti ameagiza Mwaipaya afikishwe kortini Novemba 2, 2026, saa 5:00 asubuhi. Katika amri hiyo, Jaji ameagiza wajibu maombi hao wafika mahakamani siku hiyo wakiwa na hati halisi ya kuzuiliwa kwake na kueleza sababu kwa nini mtu huyo asiachiliwe huru mara moja kutoka kizuizini anakoshikiliwa.

Wajibu maombi katika maombi hayo mbali na IGP Kenya, ni Nationa Police Services, Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai (DCI), Mkugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama (NIS) nchini Kenya. Wengine ni Mkuu wa Kituo (OCS), Kituo cha Polisi cha Ruai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wa Kenya pamoja na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu yenye kudai kuwa na maslahi ya maombi hayo.

Uamuzi huo umetolewa baada ya Taasisi ya Vocal Africa na mashirika mengine ya kutetea haki za Binadamu nchini Kenya kufungua maombi hayo Mahakama Kuu kwa hati ya dharura dhidi ya IGP na watu wengine 13. Maombi hayo yalitaka mahakama kuagiza IGP na vyombo vingine vya usalama nchini humo, kuhakikisha wanamfikisha mahakamani, Mtanzania Twaha Mwaipaya, akiwa hai au amekufa.

Jaji Muteti amesema wajibu maombi namba 1, 2 na 3 wanaamriwa hapa, wao wenyewe au kupitia maofisa wao walioteuliwa ipasavyo, kumleta Twaha Mwaipaya akiwa hai au amefariki mbele ya mahakama hii Novemba 2 saa 5:00 asubuhi.

Key points

  • Mahakama Kuu ya Kenya imeamuru IGP na vyombo vya usalama kumfikisha Twaha Mwaipaya, mtanzania aliyekutwa na watu wasiojulikana Nairobi, akiwa hai au amekufa.

Share this story

Written by

SaharaWire Newsroom
SaharaWire

Reporting for SaharaWire from the Nairobi bureau.